Mwendesha Mashtaka wa Serikali Nchini Gabon, Andre-Patrick Roponat amesema Noureddin Bongo Valentin ambaye ni Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Gabon aliyeondolewa madarakani, Ali Bongo Ondimba na washirika wake kadhaa wamewekwa kizuizini baada ya kushitakiwa kwa tuhuma za rushwa.

Mtoto huyo, sambamba na Msemaji wa zamani wa Rais, Jessye Ella Ekogha, pamoja na watu wengine wanne walio karibu na Kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani, wameshtakiwa katika Mahakama ya jijini Libreville na kuwekwa kizuizini kwa muda, ili kupisha uchunguzi dhidi ya shutuma zinazowakabili.

Noureddin Bongo Valentin. Picha ya Dreshare.

Ali Bongo Ondimba mwenye umri wa miaka 64, ambaye alitawala taifa hilo la Afrika ya Kati lenye utajiri wa mafuta tangu mwaka 2009, alipinduliwa na viongozi wa kijeshi Agosti 30, 2023 muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa Rais.

Matokeo ya uchaguzi huo yalitajwa na upinzani na Viongozi wa Mapinduzi ya Kijeshi kuwa ni ya udanganyifu na pia wakiutuhumu utawala wake kuwa umejaa ufisadi na machaguo mabaya ya Viongozi wa Serikali, ambapo siku ya mapinduzi, Wanajeshi hao walimkamata mtoto wa kiume wa rais Bongo na maafisa watano wa baraza la mawaziri.

Shigela aipongeza GGML kudhamini maonesho ya Madini
Msitumie nguvu fuatilieni maendeleo ya Watoto - ACP Abwao