Mchekeshaji anayeandika vichekesho katika kipindi cha Saturday Night Live nchini Marekani, Katie Rich amesimamishwa kazi baada ya kuandika ujumbe uliomkejeli mtoto wa Rais Donald Trump, Barron, kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter uliosomeka kuwa “Barron atakuwa mtu wa kwanza mshambuliaji hapa nchini aliyepokea elimu yake nyumbani.”
Mwandishi huyo aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter Ijumaa, ambapo ujumbe huo wa utani umeonekana kutania matumizi ya silaha Marekani, ambapo kumeripotiwa visa kadha vya raia wa Wamarekani kuwaua watu wengi kwa kuwapiga risasi.
Taarifa kutoka ndani ya SNL zimesema Katie Rich amesimamishwa kazi kwa muda usiojulikana.
Aidha, imeelezwa kuwa Barron hahudhurii masomo yake nyumbani bali husomea shule ya kawaida, tofauti na ujumbe wa mwandishi huyo unavyoashiria.
Mwandishi huyo alishutumiwa vikali mtandaoni kutokana na ujumbe huo hali iliyopelekea kufuta ujumbe huo na kuufanya ukurasa wake wa Twitter kuwa wa faragha.
Kufuatia ujumbe huo, Mwandishi huyo wa vichekesho alirejea mtandaoni Jumatatu na kuomba msamaha.