Mtu mmoja nchini  Nigeria aliyekuwa amekamatwa kwa kumuita mbwa wake jina la rais Muhamadu Buhari ameachiliwa huru bila ya kushtakiwa mara baada ya kugundulika kuwa hana hatia.

Joe Fortemose Chinakwe alitoa utetezi wake kuwa hakuwa na lengo la kumkashifu rais Buhari alipomwita mbwa wake jina la rais huyo.

Nilimuita mbwa wangu jina la rais kwa sababu yeye ni shujaa wangu.Nilianza kumpenda Buhari wakati alipokuwa  mwanajeshi hadi leo ambapo amekuwa rais.baada ya kuona  maamuzi anayochukua  dhidi ya ufisadi unaodidimiza uchumi wa taifa hili ,niliamua kulibadilisha jina la mbwa wangu  nikamuita Buhari.Sikujua kwamba nilikuwa nafanya makosa kwa kumpenda Buhari

Ummy Mwalimu Amuaga Mwakilishi Wa Shirika La Umoja Wa Mataifa UNFPA
Video: Hapi kumsimamisha Mganga Mkuu Mfawidhi Hospitali ya Mwananyamala