Mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, Felicien Kabuga, ambaye alikuwa mafichoni kwa muda wa miaka 26 kabla ya kukamatwa siku chache zilizopita nchini Ufransa amekanusha mashitaka ya kuhusika na mauaji hayo.
Kabuga mwenye umri wa miaka 84 jana Jumatano kupitia mkalimani aliimbia Mahakama ya Ufaransa kuwa, “yote haya ni urongo, sijaua Watutsi wowote, nilikuwa nafanya kazi nao.”
Mshukiwa huyo anakabiliwa na makosa saba yakiwemo ya uchochezi wa mauaji ya kimbari, jinai dhidi ya binadamu na kuunda na kufadhili kundi la wanamgambo wa kikabila ambalo lilitekeleza mauaji hayo ya kimbari ya 1994.
Mahakama hiyo ya Ufaransa ilikataa kumuachia huru Kabuga ambapo Mawakili wake walikuwa wameiomba mahakama hiyo imuachie huru kwa dhamana kutokana na hali yake mbaya ya kiafya na imuweke chini ya uangalizi wa korti.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa na polisi mjini Paris mapema mwezi huu, baada ya kuukwepa mkono wa sheria kwa zaidi ya miaka 26.