Mtuhumiwa wa ugaidi, Ally Uratule aliyekuwa anashikiliwa na jeshi la polisi jana alijirusha kutoka ghorofa ya tatu kwa lengo la kujiua au kutoroka lakini aliambulia majeraha.

Kamanda wa jeshi la polisi Kanda Maalum Ya Dar Es Salaam, Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa kuwa mtuhumiwa huyo alijirusha kutoka ghorofa ya tatu ya jengo la makao makuu ya polisi alipokuwa akishikiliwa kwa mahojiano na maafisa wa upelelezi.

“Alijirusha kutoka ghorofa ya tatu hadi chini baada ya kuaga anakwenda msalani,” alisema Kamanda Kova na kuongeza kuwa mtuhumiwa huyo alijeruhiwa na baada ya kukamatwa alipelekwa hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

Kwa mujibu wa Kamanda Kova, mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa madai ya kuhusika katika matukio ya uvamizi wa vituo vya polisi na kutekeleza mauaji. Aanadaiwa kuwa alikuwa msuka ramani na njama ya kuvamia vituo vya Ikwiriri, Stakishari na Kimanzichana.

 

Shetani Aingilia Mapenzi Ya Lil Wayne Na Christina Milian
Ibe Aimwaga Rasmi Nigeria