Mtumishi wa Halmashauri Wilaya ya Kilosa Idara ya Maendeleo ya Jamii Emerician Temu (45) aliyeuawa Julai 17 mwaka huu Nyumbani Kwake Mamboya Kata ya Mkwata Wilani Kilosa atazikwa hii leo Marangu Mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza mara baada ya kufanyika ibada ya kuaga mwili iliyofanyika kanisa la KKKT usharika wa Bungo Dayosisi ya Morogoro mdogo wa marehemu Samwel Temu amesema marehemu ameagwa jana Julai 20, 2023 kabla ya kuanza kwa safari ya Marangu.

Amesema kwa kipindi chote cha uhai wake marehemu hajawahi kusema kama ana mgogoro na mtu yoyote hivyo tukio hilo limewahuzunisha wana familia na kuiziachia mamlaka husika kufanya uchunguzi kubaini nani amehusika na tukio hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kilosa, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya, Shaka hamdu Shaka amesema kitendo alichofanyiwa mfanyakazi huyo ni ukatili mkubwa hivyo serikali inawahakikishia wananchi waliohusika wote wanakamatwa .

Taarifa za kuuawa kwa Emerician Temu zilifahamika Julai 17 usiku baada ya siku hiyo kutoonekana kazi na simu yake kutopatikana ndipo wafanyakazi wenzake walifika nyumbani ili kujua kilichomsibu ndipo wakakuta amelala chini damu zikiwa zimetapakaa sakafuni na Mwili wake ukiwa na majeraha katika nyumba hiyo aliyokua akiishi peke yake.

Mkate wenyewe umeoza - Odinga amjibu Ruto
Young Africans yasajili 21 Kimataifa