Mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Hassan Abuu Twalib maarufu kama Kiringo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 13 baada ya kumuwekea dawa za kupoteza fahamu.
Kamanda wa Polisi mkoani Unguja Magharibi Mjini, Hussein Nassir Ali, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kikatili dhidi ya mtoto huyo.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo alijaribu kutoroka akielekea Mwanza, ndipo polisi walipomkamata maeneo ya uwanja wa ndege Zanzibar na kumuweka hatiani.
“Mlalamikaji (54), jina lake nalihifadhi, alikuja kutoa malalamiko kuwa mtoto wake alichukuliwa na Kiringi na kumpeleka katika nyumba iliyokuwa haijamalizwa kujengwa huko Fukoni uwandani ambapo inadaiwa alifanikiwa kumlawiti baada ya kumpa dawa za kupoteza fahamu na kumsababishia maumivu sehemu zake za siri za nyuma”, amesema Kamanda Nassir.
-
Polisi yawaita viongozi Saba Chadema kuhusu uchaguzi Kinondoni
-
Video: Machozi ya Akwilina, Mbowe na vigogo sita waitwa polisi
-
Wanafunzi wa kike wawatoroka Boko Haram shuleni
Aidha, Kamanda Nassir amesema uchunguzi wa madaktari ulithibitisha kuathirika sehemu za siri za nyuma za mtoto huyo.
Kwa upande mwingine, Kamanda Nassir amesema ameunda timu ya uchunguzi iliyojumuisha wakuu wa upelelezi wa wilaya tatu wilaya ya mjini, wilaya ya Magharibi A na B ili wakachunguze ukweli wa tukio zima lilotokea.