Kamishna wa Polisi Utawala Menejimenti ya Rasilimali watu, Suzan Kaganda amewaomba watumishi kuweka utaratibu mzuri wa kujiandaa na kustaafu pindi wanapo ajiriwa ili kuondoa msongo wa Mawazo kinapokaribia kipindi cha kustaafu.

Kamishna Kaganda ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi la Polisi kutoka Kikosi cha Bohari Kuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es salaam, ambapo amewaomba watumishi raia na askari wa Jeshi hilo kujiwekea utaratibu mzuri wa kustaafu ili kuondoa fedheha.

Ameongeza kuwa wastaafu hao ni mabalozi huko waendako baada ya kumaliza utumishi wao ndani ya Jeshi hilo huku akimtaka Boharia Mkuu Kamishna Msaidizi wa Polisi, Moses Mziray Kushirikisha askari waliostaafu ili kuwaongezea ujuzi askari wanaofanya kazi Bohari kuu ya Jeshi hilo.

Kamishna wa Polisi Utawala Menejimenti ya Rasilimali watu, CP Suzan Kaganda.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam – DPA, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Dkt. Lazaro Mambosasa amempongeza Boharia Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa namna ambavyo anashirikiana na Wakuu wa komandi nyingine huku akiwaomba wastaafu wa Jeshi hilo Kwenda kulisemea vizuri Jeshi hilo.

Nae Boharia Mkuu Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi, Moses Mziray amewataka askari wanaoendelea na utumishi ndani ya Jeshi hilo kuhakikisha wanajenga nidhamu ya ya kazi ili iwasidie kusonga mbele na kupata vyeo huku akitumia mashairi ya shabani Robart kuwakumbusha askari namna bora ya kuishi kwa nidhamu ambayo itawafanya wasonge mbele.

Akiongea kwa niaba ya wastaafu waliomaliza muda wa utumishi ndani ya Jeshi la Polisi, Salima Mussa amewashukuru Maofisa na askari wa vyeo mbalimbali aliofanya nao kazi kwa karibu huku akisisitiza kuwa nidhamu ya kazi ndio msingi wa mafaniko yake kufikia hatua ya kustaafu bila kupata mashtaka ya kijeshi ndani ya Jeshi hilo.

Kampeni Afya, Maisha Bora yaunga mkono juhudi za Serikali
Upatikanaji wa haki unataka ushirikiano - Hamdun