Moja kati ya waasisi wanaotajwa kuwa waasisi wa TANU na CCM, Mzee Augustino Kishumbuo, alitangaza kuhamia rasmi Chadema na kurudisha kadi ya CCM aliyoipata Aprili 30 mwaka 1977.

Akitoa sababu za kuhamia Chadema, Mzee Kishumbuo ambaye ni mkazi wa Moshi vijijini mwenye umri wa miaka 86, alisema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo kwa kuwa anaona chama chake cha zamani (CCM) kimepoteza muelekeo.

“Nimefanya uamuzi huu mgumu kwa sababu nimesoma alama za nyakati kuhusu anguko la la CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Chama change caha zamani kimepoteza mwelekeo, nikaamua kuyafuata mabadiliko yalipo,” Mzee Kishumbuo kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge wa jimbo la Moshi Vijijini kwa tiketi ya Chadema, Anthony Komu.

Uamuzi wa Mzee huyo ulionekana kumtia nguvu Anthony Komu aliyedai kuwa hizo ni dalili zinazoonesha wazi kuwa atamshinda mpinzani wake wa CCM katika kinyang’anyiro cha ubunge wa jimbo la Moshi Vijijini, Dk. Cyril Chami aliyekuwa waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara.

“Siuoni tena ushindi wa CCM  katika jimbo hili… mshindani wangu amekata tama kwa sababu timu yake ya kampeni imesambaratika, kabla ya wananchi hawajamwadhibu kwa kura,” alisema Komu katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika wikendi iliyopita.

Mzee Kishumbuo mwenye umri wa miaka 86 alitangaza kuihama CCM siku moja kabla ya moja kati ya wanasiasa wakongwe waliofanya kazi katika nafasi ya ngazi za juu za TANU na CCM, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru mwenye umri wa miaka 85 kutangaza kuachana na CCM akitoa sababu kama alizozitoa mzee Kishumbuo.

 

 

 

 

Mourinho: Nitaondoka Wachezaji Wakinikataa
Nyota Ya Jaha Huenda Ikawakia Jangwani 2015-16