Kiungo kutoka nchini Ghana Mubarak Wakaso amenusurika kwenye ajali ya gari, akiwa nchini Hispania mapema jana jumapili.

Kiungo huyo wa klabu ya Deportivo Alavés alikua akielekea uwanja wa ndege wa mjini Bilbao (Loiu airport), kwa ajili ya kuanza safari ya kurejea nchini kwao Ghana, tayari kwa maandalizi ya timu ya taifa ambayo itakabiliwa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika 2019 (AFCON 2019) dhidi ya Sierra Leone.

Wakaso mwenye umri wa miaka 28, alipata ajali hiyo, saa kadhaa baada kuisaidia klabu yake kuibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya mabingwa wa soka barani Ulaya (Real Madrid).

“Nipo salama, ninamshukuru sana mungu.” Alisema Wakaso baada ya kunusurika kwenye ajali hiyo ya gari.

Uongozi wa klabu yake pia ulithibitisha kunusurika kwa wakaso kupitia tovuti ya klabu:  “Wakaso Mubarak amenusurika na ajali, yupo salama,” ilieleza taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu.

“Wakaso aliendelea na safari yake ya kuelekea uwanja wa ndege dakika kadhaa baadae, na alifanikiwa kusafiri kurejea nyumbani kwao Ghana.”

Image result for mubarak wakaso car accidentGari la Mubarak Wakaso baada ya kupata ajali.

Kiungo huyo amerejeshwa kwenye kikosi cha kocha Kwesi Appiah, ambacho kitakua ka kazi kubwa ya kufanya katika michezo miwili mfululizo dhidi ya Sierra Leone, itakayochezwa Oktoba 11 na 15.

Katika mchezo uliopita kikosi cha Ghana kilikubali kupoteza kwa kufungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya Kenya mjini Nairobi.

Wengine waongezwa tuzo ya Ballon d'Or
Watano watajwa kinyang'anyiro cha Ballon d'Or