Baada ya kuachana na Azam FC na muda wa mjuma mawili kupita, Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Mudathir Yahya ameibuka na kutangaza msimamo wake.
Kiungo huyo ameachana na Azam FC, baada ya kuitumikia Klabu hiyo ya Chamazi-Dar es salaam kwa zaidi saba, amesema kwa sasa amedhamiria kuupumzisha mwili wake huku akiwa na karibu na familia.
Amesema amechukua maamuzi hayo kwa matakwa binafsi, huku akiamini muda utakapowadia atarejea tena Uwanjani na kucheza kwa juhudi kama ilivyokua akiwa Azam FC na Singida United.
Amekiri kupokea ofa kadhaa katika klabu za Tanzania, lakini anaheshimu maamuzi aliyoyachukua kwa sasa, na huenda akarejea tena dimbani kupitia Dirisha Dogo la Usajili.
“Nina uwezo wa kucheza msimu huu kwani dirisha bado halijafungwa na nimepata ofa kutoka timu mbalimbali ambazo nimezifahamisha kuwa nahitaji Kupumzika kwa muda hadi dirisha dogo litakapofunguliwa.”
“Naifahamu vizuri ligi ya Tanzania kwani nimecheza muda mrefu zaidi kuachwa na Azam FC haina maana kwamba kiwango changu kimeshuka nipo vizuri na naweza kucheza timu yopyote ambayo inaweza kunisajili.” amesema Mudathir