Wakati dili ya Mbwana Samatta kwenda KRC Genk ikiwa bado haijatoa majibu yanayo eleweka, nyota ya straika huyo ambaye ni Mchezaji Bora wa Afrika (ligi ya ndani) imeendelea kung’ara baada ya vigogo wa Ligi kuu ya Ufaransa, Olympic Marseille nao kujitosa kumuwania.

Akiwa nchini DR Congo kwenye klabu yake ya TP Mazembe ambako ameenda kwa lengo kuu la kumshawishi Bosi wake Moise Katumbi akubali kumuuza Genk, Samatta amepokea simu ya Rais wa Marseille inayomtaka kukaa mkao wa kula kwa maana muda wowote anaweza kuitwa kwenda kuvaa jezi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka jijini Lubumbashi ni kwamba Samatta amezungumza na bosi wa vigogo hao kwa njia ya mtandao wa Skype na kwamba ameambiwa kuwa wanahitaji straika wa aina yake ila chaguo lao la kwanza ni Muivory Coast anayekipiga CSKA Moscow ya Urusi, Seydou Doumbia ambaye wapo kwenye mazungumzo naye.

Kama Doumbia atagomea dau la Marseille, wafaransa hao watalazimika kumtumia tiketi haraka Samatta ili akamalizane nao kabla dirisha la usajili halijafungwa rasmi.

Hata hivyo mtandao huu unajua kuwa mpango wa Samatta kwenda Genk uko kwenye hatua za mwisho na kwamba muda wowote Mfungaji Bora huyo wa ligi ya Mabingwa Afrika atakwea pipa kwenda Ubelgiji

Rais Magufuli amtimua Mkurugenzi wa NIDA, Mabilioni yalitumika ndivyo sivyo
Bale Akanusha Uvumi Uliosambwazwa Kwa Makusudi