Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amepanga kukutana na aliyekuwa Makamu wake, Emmerson Mnangagwa ambaye alimfuta kazi na kusababisha vuguvugu la mgogoro wa madaraka nchini humo.

Taarifa ya mkutano kati ya wawili hao imetolewa jana na Mkuu wa Majeshi ya Zimbabwe, Constantino Chiwenga ikiwa ni siku chache baada ya jeshi kuingilia kati mgogoro huo.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Majeshi, Mnangawa atawasili nchini humo muda wowote kuanzia jana kwa ajili ya mazungumzo hayo.

Aliwataka wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati viongozi wao wakitafuta suluhu kwa maslahi ya Taifa hilo.

Jeshi hilo limewataka viongozi wa Zanu-PF, Wapigania uhuru,vyama vya  upinzani na wanafunzi kuhakikisha wanajiepusha na vitendo ambavyo vinaweza kuhatarisha amani.

Mugabe ambaye alikuwa anatarajiwa kujiuzulu, alionesha kutokuwa na mpango huo kupitia hotuba yake kwa Taifa hilo akiwataka watu kusameheana na kurejesha hali ya utulivu iliyokuwepo.

Ramos aachwa kikosi cha Real Madrid
Nyalandu kikaangoni Takukuru