Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amepuuzia  taarifa za hivi karibuni za uvumi juu ya afya yake, kwa kusema kwamba alikufa na akafufuka.

 Mugabe mwenye umri wa 92, aliyasema hayo alipokuwa akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Harare akitokea nje ya nchi.Taarifa ya safari yake ilisema kuwa ndege yake ilikuwa ikielekea mashariki mwa Asia, na kwamba badala yake ilikwenda Dubai.

Mwezi Mei, Mke wa Mugabe, Grace, alisema kuwa mumewe ataongoza nchi hata akiwa kaburini.

Taarifa za uvumi kuhusu safari zake za ndege na nyinginezo, zilisababisha kuenea kwa tetesi kwamba afya ya  Mugabe ilikuwa mbaya na kwamba alikwenda Dubai kwa matibabu ama hata alikuwa tayari amepoteza maisha.

Tovuti ya Gazeti linalochapishwa kila siku la Southern Daily, liliandika makala yenye kichwa cha habari “Robert Mugabe anaumwa kiharusi, Mnangagwa sasa ndie rais wa mpito wa Zimbabwe”.Emmerson Mnangagwa ni makamu wa rais wa Zimbabwe.

Wanusa Jela kwa kumpa dawa za kulevya mtoto wao wa miezi 4
Magufuli ataka Shein amuadhibu Maalim Seif, aeleza ambacho angemfanya kwa kugoma kumpa mkono