Kamati ya Migodi na Nishati ya Bunge la Zimbabwe imeeleza kuwa itamwita Rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe kufafanua kuhusu upotevu wa almasi yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 15 kutoka eneo la almasi la Marange.
 
Gazeti la Herald Jumatano wiki hii lilimnukuu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Temba Mliswa akisema kamati yake imekamilisha taratibu za kumwita Mugabe mbele ya kamati hiyo kufafanua kuhusu nini hasa kimetokea katika sekta ya almasi. 
 
“Hoja yangu ni kuwa kinachofanyika si kumwandama Mugabe au yeyote bali tunachotaka ni kupata majawabu kuhusu upotevu wa almasi zenye thamani ya dola za Marekani bilioni 15,”amesema Mliswa
 
Hata hivyo, Vyombo vya habari nchini Zimbabwe vimeeleza kuwa maofisa kadhaa waandamizi wa serikali iliyopita pamoja na wenzao katika vyombo vya usalama wamekwishaitwa mbele ya kamati hiyo ya Bunge na kujieleza kuhusu upotevu huo wa almasi ya kiwango hicho cha fedha.
 
  • Zuckerberg aliomba radhi bunge la Marekani
  • Trump aitaka Urusi kujiandaa na mashambulizi
  • Waandishi wang’ang’aniwa Gerezani

Spika abadiri utaratibu wa kuingia Bungeni
Waandishi wang'ang'aniwa Gerezani