Bunge la Zimbabwe limetoa tamko juu ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe, kumsweka gerezani iwapo hatajiwasilisha mbele ya kamati ya bunge inayotaka kumfanyia uchunguzi juu ya shutuma inayomkabili ya ufujaji wa dola bilioni 15 za ushuru uliotoka kwa mauzo ya Almasi.
Hata hivyo Rais Mugabe alipuuza agizo hilo la Bunge lililomtaka afike bungeni mbele ya kamati kutoa maelezo juu ya ufujaji wa pesa hizo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Temba Mlisa amesema Bunge litamwandikia barua ya mwisho likimkumbusha juu ya kufika bungeni hapo mbele ya kamati hiyo.
Amesema ””Tunatumai kwamba barua hii ya mwisho itakuwa kitu ambacho atafurahia. Iwapo hatafika mbele ya kamati hii, atakuwa amedharau bunge…na kuna athari kadhaa za kufanya hivyo. Wacha Hebu wakumbusheni kwamba mbunge Roy Bennet, ambaye kwa sasa ni marehemu, alifungwa jela kwa ushauri wa bunge. Kwa hivyo tusisahau nguvu za bunge hili,” aliongeza mwenyekiti huyo.
Hii ni mara ya pili kwa Mugabe, mwenye umri wa miaka 94, kukosa kufika mbele ya kamati hiyo ili kujibu maswali.
Kamati hiyo inachunguza shutuma za ufisadi katika seka ya madini aina ya almasi. Mnamo mwaka wa 2016, Mugabe na Zimbabwe walipoteza dola bilioni 15 kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ufujaji katika sekata hiyo.
Madini ya almasi yaligunduliwa nchini Zimbabwe mnamo mwaka 2006 na kuleta matumaini kwamba uvumbuzi huo ungesaidia kuimarisha pakubwa uchumi wa nchi hiyo uliodorora mno.