Mwili wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe unaotarajiwa kuzikwa jumapili hii septemba 14, nchini humo unatarajiwa kuagwa siku ya jumamosi.

Mwili huo unatarajiwa kurejeshwa nchini Zimbabwe kesho kutoka Singapore alipokuwa akipatiwa matibabu hadi umauti ulipompata.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mpwa wa marehemu Mugabe, familia yao bado haijafahamu Rais huyo wa kwanza wa Zimbabwe atapumzishwa wapi, japo wanaamini mazishi yatafanyika katika makaburi ya Mashujaa ya Taifa, kama ilivyokuwa imepangwa kabla ya kuondolewa madarakani mwaka 2017.

Katika makaburi hayo ya mashujaa yaliyojengwa kwa msaada wa Serikali ya Korea kaskazini, ndipo alipozikwa mke wake wa kwanza, Sally Mugabe ambaye alikuwa ni moja ya wanaharakati wa ukombozi wa Zimbabwe, aliyetazamwa na wengi hadi kifo chake kama ni mama wa Taifa la Zimbabwe.

Aidha taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo, zinaeleza kuwa baadhi ya ndugu zake wanataka azikwe kijijini kutama, alipozaliwa katika jimbo la Magharibi mwa mji mkuu, Harare.

 

Amkata mapanga mpenzi wake siku moja kabla ya kumtambulisha ukweni
Tundu Lissu afunguka baada ya kukwaa kisiki Mahakamani