Mgombea anaewania nafasi ya kuwa rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa endapo atafanikiwa kuwa rais wa nchi hiyo atahakikisha anawafunga jela rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe na mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni.

Trump alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipokuwa Washington DC ambapo aliwataka viongozi hao kufahamu kuwa siku zao zinahesabika.

“Mugabe na Museveni wanapaswa kufahamishwa kuwa siku zao zinahesabika na kwamba nitawakamata na kuwafunga jela. Kama viongozi waliopita wa Marekani walishindwa kuwazuia hawa madikteta wawili. Mimi binafsi nitafanya hivyo,” alisema Trump.

“Mugabe na Museveni wameshaipatia dunia matatizo ya kutosha na sasa ni muda wa mtu kuumaliza ukichaa huu ili amani itawale,” aliongeza.

“Kama Obama anawaogopa, Sitawaogopa. Kama Clinton na Bush waliwaogopa, kama Papa anawapigia magoti, sitaweza kushushwa hadi kwenye ngazi hiyo. Sitakuwa muoga daima. Ninaahidi kusafisha matatizo yote ya kisiasa duniani na kuhuisha haki za kimataifa,” alijigamba.

 

Azam FC Wanatazamwa Kama Silaha Kwa Yanga
Mabalozi wa Iran watimuliwa Katika nchi Hizi