Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe leo ameondoka nchini humo kwa mara ya kwanza tangu ajiuzulu nafasi hiyo akielekea nchini Singapore kupata matibabu.

Kwa mujibu wa gazeti la News Day la nchini humo, Mugabe anaelekea Singapore na baadae ataenda Malaysia kumsalimia binti yake ambaye ni mjamzito.

Mugabe ameambatana na mkewe Grace pamoja na baadhi ya maafisa wa Serikali.

Msemaji wa Rais Emmerson Mnangagwa, George Charamba amesema kuwa ofisi ya Rais haifahamu lolote kuhusu safari ya Mugabe na kwamba haina mawasiliano yoyote na timu yake.

Mugabe alilazimishwa kujiuzulu nafasi ya urais baada ya jeshi kuingilia kati mgogoro wa uongozi wa chama hicho na kutangaza kuwasaka na kuwaondoa maadui waliokuwa wanamzunguka.

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 13, 2017
Lissu: Nitadai haki mpaka mwisho wa maisha yangu