Mshambuliaji kutoka DR Congo na Klabu ya Simba SC Chriss Mutshimba Koppe Mugalu amesema anaamini katika uwezo wake, na hatetereshwi na taarifa za kuwa kwenye orodha ya wachezaji ambao huenda wakaondoka Msimbazi.

Mugalu amekua kwenye wakati mbaya katika kipindi hiki, kufuatia Klabu ya Simba SC, kutakiwa kupunguza idadi ya wachezaji watatu wa kigeni, huku jina la Mshambuliaji huyo likiwa miongoni mwa wanaotajwa huenda wakachwa.

Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa na Simba SC akitokea Power Dymano ya Zambia miaka miwili iliyopita, amesema naamini ana uwezo mkubwa wa kucheza soka na kufunga, na ana matarajio makubwa ya kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC msimu ujao.

Amesema endapo itatokea anaondolewa klabuni hapo atakua tayari kuondoka na kwenda sehemu nyingine, ambako anaamini atacheza na kuendelea kudhihirisha ubora wake.

“Naamini katika uwezo wangu. Msimu ulioisha ni changamoto tu za majeraha hadi kushindwa kufanya vizuri, kama nikibaki hapa nitarudi kwenye makali yangu au nikiondoka nitaenda kuonyesha ubora huko.”

“Maisha ya mchezaji soka ndio yalivyo unaweza kuwepo kwenye timu ama ukaondoka. Hapo sina wasiwasi na lolote kati ya hayo mawili kuondoka ama kubaki, kwani naamini kwenye uwezo wangu.” amesema Mugalu

Kwa sasa Mugalu yupo Kambini Ismaili-Misri akiwa na wachezaji wenzake wa Simba SC, kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na ‘CAF’.

Serikali yamfanyia ‘suprise’ mjasiriamali
Mohamed Badru kujitetea mbele ya Kamati ya Maadili