Serikali imeitaka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kuachana na kile kinachoonekana kama ujanja ujanja wa kuwasumbua wanachama wote wanaofuatalia mafao yao.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Jenista Muhagama akiwataka wakurugenzi wa mashirika hayo kuchukua hatua kwa wafanyakazi hasa mameneja wa mikoa ambao bado wanafanya kazi kwa mazoea na uzembe.
Waziri Muhagama ameeleza kushangazwa na kitendo cha wafanyakazi wa mifuko ya hifadhi kuwadai barua za miaka 40 nyuma wanachama wanaostaafu kama moja ya vielelezo.
Mhagama amesema kuwa moja ya kazi ya mifuko hiyo ni kuweka kumbukumbu za mfanyakazi ambaye ni mwanachama wao kabla ya kufikia umri wa kustaafu, ili alipwe mafao yake bila usumbufu.