Baadhi ya watoto hapa nchini huzaliwa na jinsi tata yaani wazazi wanashindwa kujua mtoto ni wa kiume au wa kike.Habari njema kwa watanzania wote ni kuwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kushirikiana na jopo la madaktari kutoka Saudia Arabia kwa kara ya kwanza wameweza kufanya upasuaji wa kurekebisha hali hiyo.
Akizungumza katika mkutano uliohudhuriwa na mabalozi wa nchi za Falme za kiarabu (Oman na Saudi Arabia), Misri, Palestina, Kuwait na Morocco, Daktari bingwa wa upasuaji wa watoto kutoka Muhimbili, Zaituni Bokhari amesema kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji mgumu hasa kwa watu wa jinsi tata na wenye uvimbe katika mfuko wa nyongo 24.
Amesema upasuaji wa mfumo kwenye uzazi ‘jinsi tata’ umefanyika kwa watu watatu, mmoja akiwa na umri wa mika 16 ambaye awali alikuwa analelewa kwa jinsi ya kiume.
IGP Sirro alivyokimbiwa na mchumba kisa Mzawa wa Mara
Baada ya kumpima vipimo mbalimbali ikiwemo Ultra sound na DNA, amerekebishwa mfumo wake na kumuwekea mfumo wa kike ambao ndio unafanya kazi.
Amesema “Ambiguous Genitalia’ ni neno linalotumika kuelezea viungo vya siri vya mtoto aliyezaliwa ambavyo ni vigumu kujua kama ni wa kike au kiume, lakini wenzetu wamebobea kwenye utaalamu huu wametusaidia na upasuaji umefanyika kwa mafanikio makubwa”
Kufanyika kwa upasuaji huo hapa nchini kumeokoa gharama kubwa ambayo ingetumika kama wenge toka nje ya nchi, kwani wagonjwa watatu pekee iwapo wangepelekwa nje matibabu yao yangegharimu si chini ya Tsh. milioni 200 kwani gharama ya mgonjwa mmoja ni dola za Marekani 30,000.
Upasuaji huo ilianza tangu jumatatu, Mtaalamu wa upasuaji kwa watoto, Petronila Ngiloi amesema ” Mtu mmoja upasuaji umechukua saa nane na wengine ni zaidi, lakini kikubwa tumejifunza kutoka kwao (Saudia Arabia), na kupata uzoefu na mbinu zaidi za kuweza kusaidia watanzania wenzetu”.
Aidha ameiomba Serikali kudumisha zaidi ushirikiano na falme za Kiarabu ili madaktari wao waweze kuja kutoa elimu mara kwa mara ili wazawa waweze kupata uzoefu na ujuzi zaidi.
Kwa upande wa daktari bingwa kutoka Saudia Arabia, aliyeongoza upasuaji huo Emad Burhan amesema ni faraja kubwa kwao kuja nchini kufanya upasuaji kwa wagonjwa na kusaidia kuwarudisha katika hali za kawaida.
Pia amesema ni furaha kwao kuona upasuaji unafanyika kwa mafanikio makubwa kwani lengo lao ni kusaidia na kutoa ujuzi kwa madaktari wa nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania, ili kuokoa maisha ya watu wengi na kwa upande wa Tanzania wametibu wagonjwa zaidi ya 100 ikiwemo kutenganisha pacha wailioungana.