Madaktari bingwa wa Upasuaji wa watoto katika hospitali ya taifa ya Muhimbili wamekuja na teknolojia ya kufanya upasuaji kwa watoto wanaozaliwa wakiwa na tatizo la utumbo wazi, kwa kutumia utaratibu wa kuwavalisha mifuko maalumu.
Kwa mara ya kwanza hopitali hiyo wamefanikiwa kuokoa maisha ya watoto wawili waliozaliwa wakiwa na tatizo la tumbo wazi na utumbo kuwa nje.
Dkt. Zaituni Mohamed bingwa wa upasuaji kwa watoto amesema kuwa awali kabla ya teknolojia hiyo uwezekano wa mtoto anayezaliwa na utumbo nje alikuwa na asilimia 100 ya kufariki lakini baada ya teknolojia hiyo uwezekano wa kupona ni asilimia 100 .
”Kuanzia sasa mtoto akizaliwa na tatizo hilo atavalishwa mfuko maalumu unaotunza majimaji akiwa wodini ambapo kila siku watoa huduma wetu watakuwa wanasukuma utumbo kurudi tumboni kwa vipimo maalumu na katika kipindi cha siku tatu hadi tano utumbo huo utakuwa umerudi” amesema Dkt Zaituni
Ameongeza kuwa kuhakikisha huduma hii inapatikana kote nchini tayari Hospitali ya taifa Muhimbili imechukua jukumu la kutoa mafunzo kwa hospitali zote za kanda namana ya kuwapa huduma watoto wanaozaliwa utumbo je kabla ya kuwapa rufaa ya kwenda Muhimbili.