Tezi dume ni kiungo kinachopatikana katika mwili wa binadamu mwenye jinsia ya kiume na inapatikana ndani ya kibofu, mbele ya njia ya haja kubwa.

Hayo yameelezwa na daktari kutoka hospitali ya taifa ya Muhimbili, Dr. Ryuba Nyamsogoro wakati akitoa ufafanuzi juu ya tezi dume kwani watu wengi wamekuwa wakidhani kuwa tezi dume ni ugonjwa.

Amefafanua na kusema tezi dume si ugonjwa bali ni kiungo katika mwili kama viungo vingine vinavyopatikana kwenye mwili wa binadamu..

Daktari ameendelea kwa kuzitambulisha kazi kubwa mbili za tezi dume kwenye mwili wa mwanaume, ambapo amesema kazi mojawapo ni kutoa kimiminika ambacho ni muhimu katika kujenga mbegu za kiume, na ameendelea kwa kuitaja kazi ya pili kuwa inasaidia katika mlango wa ndani wa njia ya mkojo kwa kuzuia mkojo na vimiminika vingine vinavyotoka visirudi sehemu ya ndani.

Pamoja na maelezo hayo kuna ugonjwa maarufu unampata mwanaume kwenye tezi dume maarufu kama kansa ya tezi dume.

Huu ni ugonjwa unaowapata wanaume tu unaotokana na uvimbe wa tezi dume, japokuwa madaktari wanasema sio kila uvimbe kwenye tezi ni kansa.

Imeelezwa kuwa kansa hutokea pale ambapo seli za mwili zinajizalisha na kuongezeka kwa namna isiyo ya kawaida na bila kizuizi.

Kasi hii ya kukua na kuenea kwa kansa hutofautiana kutokana na mtu mmoja na mwingine ila kadri mwanaume anavyoongezeka kiumri ndivyo anavyokuwa kwenye nafasi kubwa ya kuugua ugonjwa huu.

Tatizo hili huwapata sana wanaume kuanzia miaka 60 na kuendelea, japokuwa kwa miaka ya sasaivi na mitindo ya maisha ambayo vijana wanaishi ugonjwa huu huwapata hata vijana wenye umri wa kuanzia maika 25, pia huwapata wanaume wanaokunywa pombe kupita kiasi, wanaofanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza rangi au wanaofanya kazi ya kupaka rangi, walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama, hao wanahatari kubwa sana ya kukumbwa na ugonjwa wa saratani ya tezi dume.

Dalili kubwa ya ugonjwa huu wa saratani ya tezi dume ni kupata shida unapoanza kukojoa au kujisaidia haja ndogo, kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa, kukojoa mkojo kwenye mtiririko dhaifu, kujiakkamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote, kutoa mbegu za kiume zilizochanganyika na damu na endapo sratani hiyo itakuwa imesambaa mgonjwa hupata maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni, na tatizo huenda mbali zaidi kwa uume kushindwa kusimama, uzito kupungua, kuhisi kichefuchefu na uchovu.

 

 

Hizi hapa nafasi nyingine za ajira kutoka makampuni 8 Tanzania
Waliotimkia CCM waanza kurejea Chadema