Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya China imetoa fursa ya kufungua soko la muhogo mkavu kutoka Tanzania, kitu ambacho kinafungua ukurasa mpya wa zao la muhogo kuwa miongoni mwa mazao ya biashara.

Ameyasema hayo bungeni Jijini Dodoma katika hotuba yake aliyoitoa wakati wakuahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge.

Amesema kuwa ili kuwezesha wakulima na wafanyabiashara wa Tanzania kunufaika na fursa hiyo, Mei 2018 ulisainiwa mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya China kuruhusu bidhaa za muhogo mkavu kutoka Tanzania kuingia katika soko la China.

Aidha, kufuatia hatua hiyo, mwezi Juni 2018, tani 74 za muhogo mkavu kutoka Tanzania zimeingizwa China kupitia Bandari ya Qingdao iliyopo katika jimbo la Shandong.

Hata hivyo, Majaliwa amesema kuwa kiasi cha muhogo kilichofanikiwa kuingizwa katika soko la China bado ni kidogo ikilinganishwa na mahitaji ambayo yanazidi tani 150,000 kwa mwaka.

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 30, 2018
Prof. Jay awekwa kikaangoni, atakiwa kutoa ushahidi