Muigizaji na Mtangazaji maarufu wa Ukraine Pasha Lee, 33 aliyekua akiigiza sauti katika michezo ya Maigizo ameuwawa katika vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine kwa siku ya 13 sasa.
Siku tano zilizopita kwa mujibu wa jarida la habari la Daily Mail, Pasha aliweka picha katika mtandao wake akiwa amevalia mavazi ya Kijeshi na kuandika ‘Tuungane Pamoja’.
Picha yake ya Mwishoni kwa siku mbili zilizopita aliyokuwa amehusishwa na Irpen iliandikwa ‘kwa masaa 48 yaliyoisha tunapata wasaa wa kuouga picha na kuonesha tulivyopigwa mabomu na bado tunatabasamu na ni kwa sababu tutashinda’
Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari wa Ukraine Sergiy Tomilenko, amesema Lee alikwenda kupigana kwa ajili ya nchi yake na amefariki ameacha bado vita inaendelea, na kufikisha ujumbe wa umoja wa waandishi wa habari kwa familia na wafiwa wote.
Rais wa Ukraine Volodmor Zelensky amesema analaani mapigano hayo na anaamini Mungu hatasamehe, Watu wa Ukraine hawatasahau na siku ya hukumu itafika
Alisema “hatutaweza kusahau kwa sababu kuna mama na maelfu ya watu ambao hawana hatia ila wamekua wahanga, Mungu hatasamehe hata siku moja.
Pasha Lee aliachana na kazi ya uigizaji na utangazaji mwezi Februari ambapo alijiunga na jeshi la Ukraine kupigania nchi yake dhidi ya Urusi.