Muigizaji nyota wa filamu za Hollywood aliyepata umaarufu zaidi duniani kupitia ‘Black Panther’, Chadwick Boseman amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 43.

Taarifa iliyotolewa leo na familia ya Boseman imeeleza kuwa alikuwa anasumbuliwa na saratani ya utumbo tangu mwaka 2016, na alifariki akiwa nyumbani kwake akizungukwa na familia yake.

“Mpiganaji wa kweli, Chadwick Boseman aliyeyafanya yote, akawaletea filamu nyingi mlizozipenda sana… kuanzia Marshall to Da 5 Bloods, August Wilson’s Ma Rainey’s Black Bottom na nyingine nyingi, zote zilitayarishwa wakati akifanyiwa upasuaji mara nyingi hatuko naye tena,” imeeleza sehemu ya taarifa ya familia.

Boseman alizaliwa Carolina Kusini. Alisoma katika Chuo Kikuu cha Howard jijini Washington, DC, ambapo alirejea tena mwaka 2018 na kutoa hotuba yake maarufu iliyomalizia na neno ‘Wakanda Daima’.

Wakanda lilikuwa jina maarufu la Dola ya Kifalme iliyokuwa Afrika, kwa mujibu wa filamu ya Black Panther, na Boseman alikuwa Mfalme aliyepewa jina la T’Challa.

Black Panther ilisukwa na muongozaji wa filamu, Ryan Coogler kwa bajeti ya Dola za Kimarekani Milioni 200 (200 USD) mwaka 2016, na hadi kufikia Mei 2018 iliingiza zaidi ya 1.344 Billion USD kupitia Box Office pekee, huku ikijishindia tuzo nyingi kubwa.

Watu wengi maarufu duniani wametumia mitandao ya kijamii kueleza jinsi walivyoshtushwa na taarifa za kifo cha muigizaji huyo.

Jeshi la zimamoto latoa tahadhari
Twaha Kiduku ampa kichapo Dullah Mbabe