Muigizaji maarufu wa filamu kadhaa ikiwa ni pamoja na ‘Titanic is an Epic’, Leonardo DiCaprio jana alipata nafasi ya kukutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani pamoja na Vatican, Papa Francis.

Taarifa iliyotolewa na Vatican ilieleza kuwa Papa Francis alimpokea muigizaji huyo katika geti la makao yake na kisha kufanya nae mazungumzo.

Vipande vya picha za video zilizorushwa baadae na baadhi ya Televisheni zilionesha DiCaprio akizungumza kiitaliano na baadae kubadili na kuhamia kwenye kiingereza na mazungumzo yao yalihusu mabadiliko ya tabia ya nchi duniani na mazingira kwa ujumla.

DiCaprio pia alimkabidhi kiongozi huo wa dini kitabu kilichochorwa na Mreno, Hieronymus Bosch katika karne ya 16.

leonardo-dicaprio na Papa Francis 2

Katika historia ya Kanisa Katoliki, kumewahi kuwa na viongozi wa ngazi za juu duniani wa kanisa hilo (Papa) 13 waliopewa jina la Leo.

Makaburi ya raia ya pamoja ya mamia yagundulika Burundi
Abiria abahatika kusafiri peke yake na marubani wa ndege kubwa kwa uhaba wa wasafiri