Kiungo kutoka DR Congo Mukoko Tonombe amewatoa hofu mashabiki na wanachama wa Young Africans, kufuatia taarifa za kuumia kwake zilizotolewa baada ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Tunisia uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Mukoko ametuma salamu kwa wanachama na mashabiki wa Young Africans kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa kuandika “Niko sawa sasa nilianza mazoezi tangu jana”.

Ujumbe huo umerudisha tabasamu huko Jangwani yalipo makao makuu ya klabu ya Young Africans, kufuatia kiungo huyo kuhitajika kwa udi na uvumba katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimu huu.

Young Africans ipo kwenye mbio za kusaka ubingwa wa Tanzania Bara, huku ikiachwa kwa alama 6 dhidi ya Simba SC yenye alama 67, na ni miongoni mwa timu zilizotinga kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

Kova awajibu Mashabiki, Wanachama Simba SC
Kigogo Gwambina FC ajiuzulu