Kocha Mkuu wa Timu ya taifa ya DR Congo Christian Nsengi ametangaza kikosi cha wachezaji 30 watakaoingia kambini kujiandaa na michezo ya kuwnai kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika AFCON 2021 dhidi ya Gambia na Gabon baadae mwezi huu.

Kwenye kikosi kilichotajwa na kocha huyo wapo wakongwe kama  Dieumerci Mbokani ambaye anarejea kikosinibaada ya miaka mitatu  na kiungo wa TP Mazembe Trésor Mputu ambaye kwa mara ya mwisho aliitumikia tim hiyo kwenye fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN 2019’.

Naye Jackson Muleka ambaye ahakuwa sehemu ya kikosi wakati wa mchezo dhidi ya Angola amerudishwa kama ilivyo kwa Paul- José Mpoku.

Kiungo wa vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans Mukoko Tonombe naye ni miongoni mwa wachezaji waliotajwa kwenye kikosi cha DR Congo ikiwa ni mara ya kwanza kwake.

Mshambuliaji hatari Cedric Bakambu ameachwa baada ya kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona ‘COVID-19’ sambamba na Arthur Masuaku ambaye amepatwa na majeruha.

DR Congo ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi D kwa kumiliki alama sita nyuma ya Gambia na Gabon wenye alama 7, huku Angola akburuza mkia kw kumiliki alama moja.

May be an image of text

Kim Poulsen azidisha mbinu Taifa Stars
Rais wa TFF ajiondoa FIFA