Kiungo mkabaji kutoka DR Congo na klabu ya Young Africans Mukoko Tonombe, huenda akaukosa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania, utakaochezwa leo saa kumi jioni mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri.

Young Africans waliwasili mjini Dodoma jana asubuhi, na jioni walifanya maandalizi ya mwisho kwenye uwanja wa Jamhuri, huku mashabiki na wanachama wao wakishuhudia kile ambacho kinatarajiwa kuonekana kwenye mchezo wa leo dhidi ya JKT Tanzania.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Young Africans, Hassani Bumbuli, amefunguka kuelekea mchezo wa leo, huku akieleza hali ya majeruhi ndani ya kikosi chao.

Bumbuli amesema:  “Kwa mujibu wa kocha Nabi katika kuelekea mchezo wetu wa ligi dhidi ya JKT atawakosa wachezaji wake nyota watatu waliokuwepo katika kikosi cha kwanza katika michezo iliyopita ya ligi.

“Wachezaji hao ni Tonombe yeye alipata maumivu ya bega makali, tupo naye kwenye msafara ulioelekea Dodoma kucheza na JKT katika mchezo wa ligi.

“Tumekuja naye baada ya kupata nafuu atakawepo katika mchezo ujao wa FA dhidi ya Mwadui, Ninja na Carlinhos wenyewe bado wanaendelea na matibabu na hawapo katika msafara wetu.”

Young Africans inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakifikisha alama 58 huku wapinznai wao JKT Tanzania wakiwa kwenye nafasi ya 14, wakimiliki alama 33.

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa sasa unongozwa na mabingwa watetezi Simba SC wenye alama 61.

Bares apania alama tatu za Young Africans
Mwadui FC yatangulia FDL