Wanandoa, Amina Juma na Kanuno Tano wa mkoani Tabora wameamua kujiua kwa kisa kilichotajwa kuwa wamechoka kumuuguza mtoto wao kwa muda mrefu bila mafanikio ambaye amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kichwa kuongezeka ukubwa.
Ambapo Amina aliamua kujiua kwa kunywa vidonge mchanganyiko vinavyotibu magonjwa ya binadamu na mume wake Tano kujinyonga mbali kidogo na nyumbani kwao mara tu baada ya mke wake kujiua.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Emmanuel Nley amethibitisha kutokea kwa matukio hayo mawili ya kusikitisha, akiongea na waandishi wa habari alisema.
”’Mmoja wa watoto wa familia hiyo ameugua ugonjwa wa saratani kwa muda mrefu. Baada ya kumuuguza mtoto kwa muda mrefu mama aliamua kujiua ‘’ amesema Nley.
Ameongezea kuwa mara baada ya polisi kuchukua mwili wa mwanamke huyo na kuupeleka polisi kwa ajili ya uchunguzi mume wake naye aliamua kujinyonga kwa kutumia pazia na kupoteza maisha.
Mzee Kalonga ambaye ni jirani wa familia hiyo na Diwani wa kata ya kabila Manispaa ya Tabora ameeleza kuwa mwanaume huyo alisikika akisema hawezi kuishi bila mke wake ndipo muda mfupi baadae alikwenda katika msitu ulioko jirani na yumabni kwao na kujinyonga.
Aidha chanzo cha ugonjwa wa mtoto huyo kuongezeka kichwa kimetajwa kuwa miezi miwili iliyopita aliangushwa chini bahati mbaya wakati akipokezana na wifi yake ndipo tatizo la kichwa lilipoanza ambapo walihangaika kumpeleka hospitali bila mafanikio yeyote.
Hivyo walikata tamaa na kuyapoteza maisha yao.
Aidha majirani walipohojiwa walisema wanandoa hao kabla ya kukumbwa na tatizo hilo walikuwa wakiishi vizuri na ndoa yao ina miaka mitano sasa wakiwa wamefanikiwa kuzaa watoto wawili mmoja akiwa na miaka minne huku mwingine ambaye ni mdogo mwenye matatizo ya kichwa akiwa na miezi tisa.