Muigizaji na mjasiriamali maarufu nchini Rose Alphonce anayefahamika zaidi kwa jina la kisanii ‘Muna Love’ amewashauri wanawake wote wenye dhamira ya kufanya upasuaji kwa dhamira za kuongeza maumbile kuacha kutokana na madhara ambayo ameanza kuyapata yeye.

Muna amesema kuwa kufanya hivyo ni hatari na kwamba yeye ni miongoni mwa wanawake waliowahi kuthubutu kufanya hivyo na mpaka sasa anajutia kwa kuwa anapitia magumu ambayo ameahidi kuwa utakapofika wakati sahihi atasimulia.

“Achaneni na Surgery, nitakuja kuwaeleza vitu vingi ninavyopitia. Nampenda Yesu, Nawapenda.” Ameandika.

Muna ameyasema hayo kupitia ujumbe mfupi aliouandika kwenye ukurasa wake maalum wa mtandao wa Instagram (Insta Story).

Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la kukithiri kwa wanawake wengi kutamani na wengine hata kuthubutu kufanya upasuaji maalumu kwa lengo la kuongeza maumbile yao kwa madai ya kutengeneza mvuto.

Nizar Khalfan: Tuliibana Simba kweli kweli
Ahmed Ally arusha kombora Young Africans