Risi wa Uganda Yoweri Museveni ameamuru kufungwa kwa maduka makubwa, njia tao, maduka ya vifaa, biashara zisizo za chakula, saluni, nyumba za kulala wageni na karakana za magari kwa siku 14, maeneo ambayo amesema hukusanya watu wengi.
kwamujibu wa gazeti la Daily Monitor la Uganda, amri hiyo haihusu hospitali, maeneo yanayotoa huduma za kitabibu na mashirika yanayojihusisha na masuala ya afya.
Rais Museveni pia ameahidi msaada wa chakula kwa watu ambao hawafanyi kazi kutokana na vikwazo vya kukabiliana na covid-19 na hawana uwezo wa kujipatia bidhaa hiyo muhimu.
Ametoa agizo kwa polisi kuwakamata wanasiasa watakaotoa misaada ya chakula kwa jamii na kushtakiwa kwa ”jaribio la mauaji ”.
Katika hotuba yake kwa taifa iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni usiku wa Jumatatu Museveni amepiga marufuku usafiri wa kutumia magari binafsi na boda boda kuanzia saa nne usiku.
Mtu yeyote anayehitaji huduma za dharura za kiafya kama vile kujifungua au kufanyiwa upasuaji anatakiwa kupata idhini kutoka kwa maafisa wa serikali katika ngazi ya Wilaya kabla ya kutoka nyumbani.
Rais amesema kuwa wakati serikali awali ikiweka marufuku ya watu kukusanyika, bado kumekuwa na mianya ya kusambaa kwa virusi.
Ingawa, alieleza kuwa kati ya watu 33 waliothibitishwa kuwa na maambukizi, watatu pekee walikuwa wasafiri waliopata maambukizi wakiwa safarini nje ya Uganda.