Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kwa mara nyingine amekosoa hatua ya Benki ya Dunia kuondoa ufadhili wake nchini humo, akisema shirika hilo linajidanganya ikiwa linadhani kwamba watawatia hofu Waganda.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa X Museveni alisema Benki ya Dunia ni waigizaji wa kibeberu wasio na akili na wasiojua pa kuacha.
Hatau hiyo inafuatia Benki ya Dunia kisitisha ufadhili kwa Uganda kwa sababu ya sheria tata ya kupinga ushoga iliyopitishwa mwezi Mei 2023, ambayo ilikinzana na maadili ya Benki ya Dunia.
Mapema wiki hii, Museveni alikaririwa akisema ufadhili ulioondolewa hautazuia mabadiliko ya kiuchumi ya Uganda na kwamba na utasaidia jitihada za Uganda kupunguza deni la nje na kujitegemea licha ya kuwa ina washirika kadhaa wa Magharibi.