Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni amelitaka Kanisa kumtangaza rais wa zamani wa Tanzania, Julius Kabarage Nyerere kuwa mtakatifu.

Ameyasema hayo katika siku ya maadhimisho ya siku ya Nyerere ambayo ilifanyika katika eneo la Namugongo ambapo rais huyo amewaambia wafuasi wa dini ya Kikatoliki waliohudhuria sherehe za kuadhimisha siku ya Nyerere katika eneo la Namugongo kwamba kiongozi huyo alikuwa Mkatoliki aliyejitolea.

“Sote tunajua vile mzee Nyerere alivyojitolea katika kanisa hili. Alikuwa kiongozi aliyejitolea na shujaa, kwa nini basi tusimwite Mtakatifu?, amesema Museveni

Hata hivyo, Rais Museveni ametoa wito na ujumbe huo kwa,Tanzania, Kenya na Rwanda pamoja na mataifa mengine kwa kusema kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa ni kiongozi mkubwa zaidi kuwahi kukutana naye maishani mwake.

 

 

 

 

Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Costa Rica
Baba mzazi amuua mwanae kwa Panga Saa chache kabla ya harusi