Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amekutana na Viongozi wa chama chake cha National Resistance Movement – NRM, ili kujua sababu za baadhi yao kupinga nia ya mtoto wake Generali Muhoozi Kainerugaba ya kugombea urais katika uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2026.
Museveni amefanya kikao hicho na washirika wake wa karibu na wenye ushawishi ndani ya chama wakiwemo majenerali waliopigana kumuweka madarakani ambao wamekuwq wakipnga hadharani kampeni za Generali Muhoozi kutaka kugombea kiti hicho cha urais.
Viongozi hao wenye ushawishi wa NRM wakiongozwa na Generali Mstaafu, Kahinda Otafiire wamekuwa wakisema watahakikisha kwamba Museveni anagombea mhula mwingine madarani na kwamba hawawezi kumruhusu mwanawe, Muhoozi kuiongoza Uganda.
Kupitia ukurasa wake wa twiter Muhoozi alitangaza kuwa atagombea urais huku akijiita “Standby Generator” akimaanisha mtambo mbadala wa kuzalisha umeme, wakati mfumo wa kawaida wa umeme unapozima na amekuwa akisema chama cha NRM kimeoza na hakina tena uwezo wa kuongoza Uganda.