Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kupata dawa ya virusi vya Corona ambayo imegunduliwa na wanasayansi nchini humo.

Rais Museven amesema hayo wakati akihutubia taifa hilo jana jumapili ambapo amesema wanasayansi nchini humo wamefanyia majaribio ya tiba hiyo ambayo hakutoa maelezo zaidi,

Amesema kuwa kwa sasa, madaktari wanatumia mchanganyiko wa vitu maalum ambavyo vinaongeza kinga mwilini dhidi ya virusi vya Corona.

“Wanasayansi wetu wameniambia habari njema kwamba wameunda dawa saba tofauti. Sita kati ya hizo zinafanyiwa majaribio na moja inaongeza kinga ya mwili dhidi ya virusi vya Corona.” Amesema Rais Museveni

Museveni amesema kwamba dawa hiyo imefanyiwa majaribio kwa wagonjwa kadhaa wa Corona na kupona na itaanza kutumika kikamilifu kwa watu wote Desemba 15 mwaka huu.

Ameendela kwa kusema kuwa katika mda wa siku 40, dawa hiyo itakuwa imetibu watu wengi na kuweka Imani kati yaw engine kwamba inaweza kutibu Corona na virusi vingine.

Jumla ya watu 210 wamefariki kutokana virusi vya Corona nchini Uganda.

Hata hivyo kampuni kadhaa nchini Marekani na ulaya zimetangaza kupata chanjo dhidi ya virusi vya Corona.

Simba SC kurudi kesho Jumanne
Jaji Mkuu: Vijijini wanahitaji huduma za kisheria

Comments

comments