Mmmiliki wa vyombo vya habari vya Tanzanite Cyprian Musiba ameazimia kwenda mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi wa mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam uliomtaka kumlipa sh bilioni 6 aliyekuwa waziri wa Mambo ya Nje Benard Membe.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji De-Mello octoba 28 baada ya Kesi ya kutoa kashifa kusikilizwa katika mahakama kuu ya Kanda ya Dar es Salaam.

Wakili Mafuru Mafuru amesema Mwanaharakati Musiba na weenzake wamewasilisha notisi ya Rufaa hiyo tarehe 4 Novemba 2021, na wanasubiri kuitwa.

Kupitia barua yao warufani wameomba wapewe nakala za mwenendo wa kesi, hukumu, amri pamoja na vielelezo vilivyoidhinishwa ili kuwawezesha kushughulikia rufaa katika mahakama ya Rufani.

Manadiplomasia Benard Membe alimshtaki Cyprian Musiba mwaka 2018 akimtuhumu kumchafua na kumuharibia sifa yake kwa kuchapisha habari za uongo latika vyombo vyake vya habari.

CHADEMA kutoshiriki uchaguzi mdogo wa Ngorongoro
Sakata la GSM lafikishwa Serikalini