Serikali imepanga kuwasilisha bungeni muswada kuomba idhini ya Bunge kuufanya kuwa Sheria inayotoa haki ya kusoma kwa watoto wa jinsia zote kwa shule ya msingi hadi sekondari na kutoruhusiwa kuoa au kuolewa.

Mpango huo umeelezwa Bungeni na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ileje, Janeth Mbene (CCM) aliyetaka kufahamu lini serikali itaanza maandalizi ya kuchukua maoni juu ya kufanya marekebisho sheria ya ndoa ya mwaka 1971.

Kadhalika, Dk. Mwakyembe alisema kuwa Serikali inaendelea na maandalizi ya mchakato wa kupata maoni ya wananchi kuhusu marekebisho ya Sheria ya ndoa.

Alisema kuwa mchakato wa kufanyia marekebisho ya Sheria hiyo ulishaanza na kwamba ulisitishwa kwa sababu Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilikuwa ikiendelea na mchakato wa kukusanya maoni ya mabadiliko ya Katiba.

Rais Magufuli amtimua Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, kwa kutochukua mshahara wake tangu 2013
Dele Alli Aingia Kwenye Kitanzi Cha FA