Malta imekuwa nchi ya kwanza miongoni mwa nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya, kupitisha muswada wa sheria unaoruhusu rasmi ulimaji na matumizi ya bangi.

Waziri wa Usawa, Uchunguzi na Ubunifu wa Malta, Owen Bonnici ambaye ndiye aliyepeleka muswada huo wa sheria katika bunge la nchi hiyo wa kutaka bangi kuruhusiwa kutumika nchini humo amesema hatua hiyo ni mafanikio makubwa.

Amesema kuwepo kwa sheria hiyo mpya kutapunguza ama kumaliza kabisa matukio ya kushtakiwa kwa watu wanaopatikana na kosa la kuvuta bangi pamoja na kupunguza uingizwaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi kinyume cha sheria.

Kwa sasa Malta inasubiri muswada huo usainiwe na Rais wa nchi hiyo ili uwe sheria na ianze kutumika rasmi.

Chini ya sheria hiyo mpya, watu wataruhusiwa kubeba bangi hadi gramu saba, kulima miti minne ya bangi kwenye nyumba zao na kuhifadhi hadi gramu hamsini za bangi iliyokauka kwenye nyumba zao.

Mbadala wa Pogba asakwa Man Utd
Kibwana Shomari: Morrison ni hatari