Nchi Urusi, Bunge limeunga mkono Muswada ambao unawapa Marais wastaafu wa nchi hiyo kinga ya mashtaka ya jinai mara baada ya kuondoka madarakani

Muswada huo ambao unawalinda Marais wa Urusi na Familia zao dhidi ya kupekuliwa na Polisi, kuhojiwa na kunyang’anywa mali zao pindi wanapomaliza ugwe ya uongozi Serikalini.

Aidha, hawatashtakiwa kwa makosa yoyote waliyofanya maishani mwao isipokuwa mashtaka ya uhaini na uhalifu mwingine mkubwa kulingana na mazingira.

Mbunge Pavel Krasheninnikov, ambaye ni mmoja wa Waandishi wa Muswada huo amesema lengo ni kumpa Rais dhamana ambayo ni muhimu kwa utulivu wa jamii na nchi kwa ujumla.

Trump amfuta kazi afisa wa uchaguzi aliyepinga madai yake
Wanaofariki kwa kunywa sumu Kilimanjaro waongezeka