Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani leo Mei 25 kimezindua mpango wa elimu ya safiri salama ikiwa ni njia mojawapo ya kuwakumbushaa madereva sheria ya kuwa na viakisi mwanga katika magari yao.

Akizungumza na madereva  katika eneo la bandari ya Dar es salaam, Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Wilbrod Mutafungwa amesema ajali nyingi zinatokea kutokana na madereva kutoweka viakisi mwanga kwenye magari yao.

“Katika eneo hili la bandari kuna magari ya kubeba mizigo, yanachukua mizigo hapa yanaishia ndani ya nchi yetu lakini mengine yanasafirisha kwenda bandari nje ya anchi za afrika mashariki na ndio maana tukaanzia kutoa elimu huku kwa sababu ni eneo muhimu, safari nyingi zinaanzia hapa,” amesema Kamanda Mutafungwa.

Amesema kuwa sheria hiyo ya viakisi mwanga imetungwa ili kumtengenezea urahisi dereva na kuepukana na ajali za barabarani ambapo viakisi hivyo ambavyo hubandikwa mbele, pembeni na nyuma ya gari vitamsaidia gari lake kuonekana hasa nyakati za usiku.

Aidha Kamanda Mutafungwa amesema endapo madereva watakiuka kuweka viakisi hivyo hatua kali za sheria zitachukuliwaa juu yake kwa kutozwa faini ya shilingi laki moja mpaka laki tatu au faini miezi sita au vyote kwa pamoja.

Hata hivyo jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani watazunguka bandari zote nchini ili kutoa elimu kwa madereva kuhusiana na sheria ya viakisi mwanga.

Rais Samia akutana na mwana wa kifalme wa Saudi Arabia
Msiruhusu wahamiaji haramu kuingia kiholela - Jenerali Mbuge