Mahakama Maalumu ya Uhalifu wa kivita ya umoja wa Mataifa imethibitisha adhabu ya kifungo cha maisha jela iliyotolewa kwa aliyekuwa jenerali wa jeshi la Waserbia wa Bosnia Ratko Mladic kwa mauaji ya halaiki ya Srebrenica baada ya miaka takribani 26 iliyopita.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la DW, Uamuzi huo wa mahakama una maana kuwa Mladic amepoteza rufaa yake ya mwisho dhidi ya hukumu yake kwa mauaji ya kimbari.

Mladic, mwenye umri wa miaka 78, ambaye baadae alifahamika kama “Mchinjaji wa Bosnia” wakati wa Vita vya Bosnia vya mwaka wa 1992 hadi 95, alitaka afutiwe mashitaka. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewashukuru majaji na wale waliohusika katika kesi hiyo kutokana na bidii yao kwa miongo mingi.

Aidha muendesha mkuu wa mashitaka wa mahakama hiyo Serge Brammertz aliukaribisha uamuzi huo na kuwaambia wafuasi wa Mladic kuwa ni wakati wa kukubali ukweli.

Rais wa Botswana kufanya ziara Tanzania
Watumiaji wa laini nyingi za simu wajiandae