Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa katika kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga,Mra Singida,Dodoma, Arusha, Manyara na Kilimanjaro
Taarifa ya TMA iliyotolewa jana imesema kuwa athari zinazoweza kujitokeza ni uharibifu wa miundombinu na mali huku baadhi ya makazi kuzungukwa na maji.
Aidha TMA imetoa angalizo la mvua kubwa kesho tarehe 30 kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro mikoa hiyo inatarajiwa kuwa na mvua kubwa ijumaa ya January 31, 2020.
Ambapo February 1, 2020 mvua kubwa inatarajiwa kunyesha kwenye kwa baadhi ya mikoa ya Rukwa, iringa, Njombe, kilimanjaro na Arusha.
”Hatari kwa maisha ya watu kutokana na maji yanayo tiririka kwa kasi na yenye kina kirefu, ucheleweshwaji wa usafiri kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kijamii” imesema TMA