Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Albert Msando amefika katika eneo liloathiriwa na mafuriko leo Ijumaa Januari 13, 2023 eneo la Kihonda mahali ambako wananchi wameathirika zaidi huku akisaidia kuokoa watu na mali zao.
Hata hivyo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wapo kwenye maeneo mbalimbali Manispaa ya Morogoro wakiendelea kuokoa watu na mali zao.
Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro kuanzia saa 9 alfajiri, zimesababisha madhara mbalimbali kwa wakazi wa mkoa huo ikiwa ni pamoja na mafuriko na foleni ya magari Barabara kuu ya Morogoro kwenda Dodoma.
Hata hivyo, mvua imeendelea kunyesha na uokoaji unafanyika.