Mvua iliyonyesha siku mbili mfululizo imebomoa madaraja matatu Wilayani Ludewa mkoa wa Njombe na kusababisha shughuli za usafirishaji kutoka Ludewa kwenda maeneo mbalimbali kusimama.
Madaraja yaliyobomolewa ni Nyapinda njia panda ya kwenda Ibumi, daraja la Muhoro, daraja la chuma la Mhambalasi linalounganisha kata ya Mkomang’ombe na Ibumi pamoja daraja la Ludewa mjini kwenda Ludewa vijijini.
Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo kwa njia Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere amesema mvua hizo zimenyesha usiku wa February 22 na 23 mwaka huu.
Mkuu wa wilaya amewataka Wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kufanya jitihada za haraka kuweza madaraja ya muda na kuanza kuanza ujenzi wa kujenga madaraja ya kudumu na tayari amefanya mawasiliano na TANROADS Njombe ili hatua za haraka zichukuliwe.