Mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha madhara makubwa kwa wananchi wa Chalinze baada ya kutokea mafuriko ambapo takribani nyumba kumi zimesombwa na maji
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amesema kuwa uharibifu ulijitokeza ni mkubwa hivyo wananchi hao waliokumbwa na tatizo hilo wanahitaji msaada wa dharula.
Aidha, Ridhiwani ametaja maeneo yaliyoathirika na mvua hizo ambazo zimesababisha mafuriko ni Chalinze Mzee, Bwawa la umwangiliaji la Msoga ambalo limetoboka na shule ya Sekondari ya Imperial.
Hata hivyo, ameongeza kuwa madhara makubwa yaliosababishwa na mafuriko hayo ni kuharibika kwa mashamba, nyumba za wananchi kuharibika na kusabishwa wananchi kukosa pa kulala hivyo amesema wananchi hao wanahitaji kusaidiwa.