Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua iliyonyesha jijini Dar es Salaam, Pwani, Tanga,Morogoro, Unguja na Pemba imetokana na mgandamizo mdogo wa hewa katika eneo la Bahari ya Hindi.

TMA imesema mgandamizo huo umesababisha kuvuma kwa upepo wenye unyevunyevu kutoka baharini na kuelekea maeneo ya Pwani .

Aidha mamlaka hiyo imesema mvua hizo ni fupi na kwamba zitapungua leo Oktoba 14,2020 na kuongezeka kidogo Kesho Oktoba 15,2020.

Mamlaka hiyo imesema kuwa mvua za vuli katika maeneo ya pwani ya kaskazini na nyanda za juu kaskazini Mashariki zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Novemba 2020.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 15, 2020
Razak Abalora atua Asante Kotoko ya Ghana

Comments

comments