Mvuvi wa samaki, Maro Mwikwabe mwenye umri wa miaka 35, ameliwa na mamba akiwa anavua katika Mto Mara.

Mwikwabe, mkaazi wa kijiji cha Borenga Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara alitafunwa na Mamba na mwili wake ulikutwa ndani ya mto huo, Mei 25, 2019.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Juma Ndaki alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mabaki ya mwili wa Mwikwabe yalihifadhiwa kwenye Hospitali Teule ya Nyerere na kwamba ndugu wameruhusiwa kuendelea na taratibu za mazishi.

“Tumeruhusu ndugu kuuchukua mwili kwa ajili ya mazishi na taratibu nyingine za kumsaka mamba huyo zinaendelea,” Kamanda Ndaki aliviambia vyombo vya habari.

Aliongeza kuwa askari wa jeshi hilo ndio wanaoendesha msako wa mamba huyo.

Kamanda Ndaki alitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kwani tayari wameshajua kuna mamba ndani ya mto huo.

Sugu afikiria namna ya kuacha muziki, ajiuliza maswali
Mahakama yasitisha zoezi la kuhesabu kura Malawi

Comments

comments